Katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya michezo yanasonga mbele hapa nchini na kuleta hamasa, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye, amemteua Yusuph Singo Omari, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, kujaza nafasi iliyo achwa wazi na Leonard Thadeo aliyehamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Aidha, Nape amefanya uteuzi huo leo kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 kifungu namba 6, (1)(b) pamoja na kifungu namba 8 cha sheria hiyo.

Kabla ya uteuzi huo Yusuph Singo Omari alikuwa Mkufunzi Mwandamizi Chuo Kikuu cha Ardhi katika masuala ya Michezo.

Hata hivyo Nape ametoa wito kwa wanamichezo na wananchi  kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Yusuph Singo Omari ili kuweza kufikia malengo ya michezo katika nchi yetu.

Ney wa Mitego: Epuka kampani ambazo si rafiki na ndoto zako
JPM awasili Simiyu, aweka jiwe la msingi Hospitali ya mkoa

Comments

comments