Waziri wa Habari,Michezo,Vijana na Utamaduni Mh, Nape Nnauye leo amezindua radio ya kijamii jijini Dar es salaam,itakayoanza kurusha matangazo katika miji mbali mbali hapa nchini na redio hiyo itakua na fursa kubwa kwa jamii kuweza kuitumia katika shughuli zake.

Aidha redio hiyo itakua Maalum kwaajiri ya shughuli mbalimbali za kijamii ambapo  redio hiyo iko chini ya udhamini wa( UNESCO)wakishirikiana na Chuo kikuu Huria Tanzania,aidha redio hiyo itakua inarusha habari mbalimbali zikiwemo za kibiashara,siasa,michezo na nk.

Kwa upande wake Mh.Nnauye aliwaasa wamilki wa radio hiyo kufuata Sheria na kanuni zinazoongoza katika tasnia ya habari, kwa kuajiri wafanyakazi wenye weledi ili kuepuka matatizo yanayoweza kusababisha na watu wasio na maadili.

Pia Mh.Nape aligusia  kuhusu kutokurushwa kwa Matangazo ya Bunge live na kusema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Matangazo hayo kurushwa na radio zote nchini hivyo  kuna utaratibu tu unaosubiliwa kurekebishwa ili kuweza kufanikisha hilo.

Hata hivyo Mh. Nape aliwaasa waandishi wa habari kufuata Maadili ya kazi ya Uandishi na kutanguliza mbele Uzalendo na maslahi nchi na si kuikandamiza serikali kwa kila kitu,ni sahihi kuikosoa serikali lakini lazima uangalie madhara yanayoweza kutokea’’Alisema Mh Nape’’.

COCA COLA WAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MASHINDANO YA UMISSETA NCHINI
Video: Serikali imeyakubali haya mapendekezo ya Mbunge Bashe