Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp, amethibitisha kuwa mshambuliaji wake Mohamed Salah atarejea uwanjani Jumatano kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napol.
Klopp amesema kuwa Salah alikuwa yupo imara  kuivaa Crysytal Palace kutokana na hali yake kuimarika ila aliamua kumpumzisha kwa ajili ya kazi nzito ya jumatano dhidi ya Napol.
“Salah yupo vizuri na ilibidi aanze kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace niliamua nimpe mapumziko ila mwisho wa siku mchezo wetu tulishinda kwani hakuwa na timu kwa muda wa siku nane alikuwa nchini Misri na mabao yalifungwa na Robert Firmino na Sadio Mane.
“Tulipaswa kufanya changuo la kumuanzisha ama kumuacha apumzike tukakubaliana tumpumzishe atarejea uwanjani Jumatano kukabiliana na Napol,” amesema Klopp.
Kutokana na kusumbuliwa na majeruhi Mo Salah alikosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace ambao Liverpool ilishinda mabao 2-1 na kuifanya izidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 37 kwenye msimamo.

RC akamata gari la kubeba maji likiwa limebeba wafanyakazi 30
Waandamanaji wachoma kambi ya jeshi ya Umoja wa Mataifa, wadai Imeshindwa kazi