Umoja wa Vyama vya Upinzani Kenya, NASA umeilalamikia Serikali na kuishutumu kwa kufanyiwa tukio la uvamizi katika moja ya ofisi zake.

Msemaji wa muungano huo (NASA), Philip Etale amesema kulikuwa na wanaume ambao wamefunika nyuso zao na kubeba kompyuta, simu za mkononi na vitabu.

Aidha serikali imekanusha kutokea kwa tukio hilo la uvamizi wa ofisi ya Umoja wa vyama vya Upinzani (NASA).

Pamoja na hayo mgombea kwa upande wa Upinzani Raila Odinga ameeleza kuwa hatokubali kushindwa ikiwa uchaguzi huo utakuwa wa haki.

Nae Rais wa sasa, Uhuru Kenyatta ameahidi kuheshimu matokeo ya uchaguzi huo wa siku ya Jumanne licha ya kila mmoja kusisitiza kuwa ataibuka mshindi.

Uchaguzi wa Kenya mara nyingi umekumbwa na ghasia. Zaidi ya watu 1000 waliuawa wakati wa ghasia baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Video: CUF washangazwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Prof. Lipumba
Korea Kusini yakubali yaishe, yataka mazungumzo yafanyike