Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans SC, Nasreddine Nabi amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuwashambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na mwamuzi wa akiba wa mchezo wa kipigo cha 2-1 cha klabu hiyo dhidi ya Ihefu FC.

Nabi aliendelea kufanya kitendo hicho hata baada ya kuonywa kwa kadi ya manjano.

Maamuzi ya adhabu dhidi ya Kocha huyo kutoka nchini Tunisia, yametangazwa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Ligi Kuu ya Bodi ya Ligi ‘TPLB’ kupitia taarifa iliyosambazwa katika Mitandao ya Kijamii leo Ijumaa (Desemba 02).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kocha Nabi amekuwa na adhabu wa kukosa michezo mitatu kwa kuzingatia kanuni 42:2 (2.1) ya Ligi Kuu ya kudhibiti makocha.

Kwa Mantiki hiyo Kocha Nabi atakosa mchezo wa Jumapili dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Namungo FC ambapo Young Africans itacheza ugenini Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, kisha mchezo wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Kurugenzi FC utakaorindimba jijini Dar es salaam

Kisa Azam FC, Mshambuliaji Coastal Union afungiwa
Gadiel Michael afungiwa Michezo mitatu