Rais wa mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG  Nasser Al Khelaifi ameingilia kati sakata la kiungo kutoka nchini Italia Marco Verratti ambaye anahusishwa na mpango wa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini kwao Italia vinadai, Veratti huenda akasajiliwa na mabingwa wa soka nchini humo Juventus ama akaelekea Hispania kujiunga na FC Barcelona.

Al Khelaifi amesema suala hilo halitowezekana na anachokihitaji kwa sasa ni kutaka kuona kikosi chake kiendelea kuwa na ubora, hivyo hatokua tayari kuona mchezaji yoyote akiondoka mwishoni mwa msimu huu.

Amesema dhamira yake ni kufanya maboresho kulingana na mapendekezo yatakayowasilishwa kwa viongozi watendaji wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, na sio kumuuza mchezaji muhimu kama Veratti.

“Verratti hatouzwa, na sijui taarifa hizo zimeibukia wapi hadi kuchukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari, sitarajii kuona mchezajai muhimu kama huyo kuondoka mwishoni mwa msimu, zaidi ya kuona maboresho yakifanyaka ili kukiimarisha kikosi chetu.” Al Khelaifi aliliambia gazeti la Mundo Deportivo.

Hata hivyo tayari Verratti aliwahi kukanusha uvumi wa kutaka kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, na aliwaambia waandishi wa habari ameshaikataa FC Barcelona tangu msimu uliopita.

Ujenzi wa Ubungo Interchange kuanza mara moja
Mawaziri 15 wa Nchi za SADC kukutana Dar kesho