Klabu ya Azam FC imeendelea kutambulisha wachezaji iliowasajili katika kipindi hiki cha Usajili kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’.

Azam FC imetangaza kumsajili Beki wa Kulia Nathaniel Chilambo, ambaye msimu uliopita aliitumikia klabu ya Ruvu Shooting.

Azam FC imemtambulisha Beki huyo kupitia kurasa za Mitandao ya Kijamii (Facebook na Instagram) kwa kuandika: Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na beki wa kulia, Nathaniel Chilambo, kutoka Ruvu Shooting.

Chilambo amesaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu, @yusufbakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, @abdulkarim.amin, wenye kipengele cha kuongeza baada ya miezi sita kutokana na kiwango atakachokionyesha.

Beki huyo, 19, anayetumia miguu yote miwili kwa ufasaha, mwenye uwezo pia wa kucheza beki ya kushoto, amekuwa na kiwango bora kabisa msimu uliopita.

RC ataka kero za wananchi zipatiwe ufumbuzi
TCRA yataka weledi kwa 'Bloggers & Youtubers'