Jumuiya ya kujihami NATO imezindua mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo hayajawahi kutokea tangu kumalizika kwa vita baridi, mazoezi hayo yanafanyika nchini Norway ni kwa ajili ya kujiweka tayari kujibu mashambulizi iwapo mmoja wa wanachama wa Jumuiya hiyo atashambuliwa.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ya kujihami (NATO), Jens Stoltenberg amesema kuwa watafanya majaribio ya uwezekano wa kujibu changamoto za kiusalama, zinazosababishwa na Urusi tangu mwaka 2014, kufuatia nchi hiyo kuitwaa kimabavu rasi ya Crimea na pia hatua zake zinazoonekana kama jitihada za kuyumbisha usalama wa mataifa ya Magharibi.

Wanachana wote 29 wa NATO pamoja na nchi washirika Sweden na Finland watashiriki katika mazoezi hayo ya ardhini, majini, angani na mitandaoni yanayoanza leo hadi tarehe 7 Novemba.

Aidha, kulingana na msemaji wa jeshi la Norway, Ivar Moen amesema kuwa tayari vikosi vyote vimeshawasili na kwamba tayari viko maeneo husika.

Hata hivyo, zoezi hilo litawajumuisha wanajeshi 50,000, magari ya kijeshi 10,000, ndege za kivita na meli 300 ili kulinda nchi wanachama kutokana na mashambulizi.

 

Wema: Nimefunga jalada la utoto, nimefunga jalada la ujinga, nimekuwa mpya
Nick Minaj aburuzwa mahakamani