Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Gewe amewataka Wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zinazodai kupanda kwa nauli.

Amesema hayo katika kipindi maalumu cha TBC ambapo amekanusha taarifa za ongezeko la nauli kwa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani yanayoanzia safari katika kituo cha mabasi cha Magufuli mkoani Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Mustafa Mwalongo amesema hakuna nauli iliyoongezeka.

Waziri Ummy: TARURA muache kukaa ofisini
RC Makalla awataka wakurugenzi kuwawezesha maafisa ushirika kutimiza majukumu yao