Rapa Nay wa Mitego ameanza kufunguka ikiwa ni saa chache baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kutangaza kumfungia kufanya muziki kwa muda usiojulikana.

BASATA walichukua uamuzi wa kumfungia Nay wa Mitego baada ya kubainika kukaidi maagizo ya Baraza hilo na kuachia wimbo mpya wa ‘Pale Kati’ usioendana na maadili ya Kitanzania.

Nay wa Mitego ametumia mtandao wa Instagram kueleza kilicho moyoni mwake, akianza kuonesha kujutia kufungiwa akidai ‘atamiss’ matamasha kubwa alizokuwa akifanya kwenye majukwaa. Hata hivyo, Nay anaoekana kutoliacha jina la wimbo wake huo uliofungiwa.

Alipost picha akiwa kwenye tamasha kubwa na kuandika, “Daaaaah..!! Nitazimiss sana hizi Show..!! #PaleKati.”

Katika hatua nyingine, rapa huyo ametumia msamiati kuwatunisha misuli wasanii wenzake akiwaonya kuwa kukaa kwake pembeni kumewapa nafasi ya kutamba lakini atakaporudi atawakalisha.

“Paka akitoka, Panya hutawala..!! Sasa akirudi watatafuta pakujificha ni kuwatafuna tu!! #PaleKati” aliandika kwenye post nyingine.

Paka akitoka, Panya hutawala..!! Sasa akirudi watatafuta pakujificha ni kuwatafuna tu!! ???? #PaleKati

A photo posted by NayTrueboy (@naytrueboy) on

 BASATA walitangaza masharti yatakayolifanya Baraza hilo kufikiria kumuondolea adhabu hiyo Nay wa Mitego ikiwa ni pamoja na kulipa shilingi milioni 1 na kuahidi kutorudia kuimba nyimbo zisizozingatia maadili ya kitanzania.

Video: ‘Conveniently rolling‘ ya Koku Gonza
JPM aanza kuinyoosha CCM