Wakati sauti ya ‘Chuma’ ya Chid Benz inaendelea kuadimika kwenye kiwanda cha Muziki nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujikita katika kujitoa kwenye matumizi ya dawa za kulevya, Rapa Nay wa Mitego ameamua kumshika mkono.

Nay amesema kuwa amekutana na Chid Benz na kuzungumza naye mara mbili na kwamba ameguswa sana anataka kumsaidia akiamini kwa uwezo wa Mungu ataweza kufanikiwa.

“Nimekutana naye mara mbili na nimekaa naye tumezungumza nadhani anahitaji msaada sana, tena sana kwa hali na mali hasa watanzania wamuombee Chid anahitaji msaada,” Chid ameiambia Dj Show ya Radio One.

“Mimi nataka kujaribu, nataka kuthubutu nikishindwa basi lakini namuomba Mungu iwe vile ninavyofikiria. Lakini sidhani kama ni kitu ambacho nakifikiria sana ila napenda kuona siku moja Chid anarudi katika hali yake,” aliongeza.

Miezi kadhaa iliyopita, Chid Benz alihudhuria matibabu katika ‘Rehab’ iliyoko Bagamoyo kwa msaada wa meneja wa Tip Top, Babu Tale. Hata hivyo, Meneja wa Rehab hiyo alidai kuwa rapa huyo aliondoka kabla ya kumaliza kipindi chote ha matibabu kilichotakiwa.

Polisi Makao Makuu watoa tamko kuhusu kupotea kwa Msaidizi wa Mbowe
Facebook yapigwa faini ya Matrilioni kwa kufanya udanganyifu