Wasanii wengi walishawahi kukumbwa na kufuli la basata kutokana na kutoridhishwa na ujumbe au picha zilizotumiwa na wasanii hao, huku kukiwa na lawama za hapa na pale kwenda kwenye baraza hilo.

Wapo wa sanii ambao walikwisha hoji juu ya vigezo vinavyotumika ikiwa zile za nje ya nchi zikiendelea kuchezwa na vituo vya hapa nchini, kufuli hilo Juma jux alishawahi kukutana nalo katika kichupa cha (uzuri wako), snura (chura),roma (viva),Nay wa mitego na wengineo wengi.

Nay

Katika ujio mpya wa sasa wa Ney wa mitego anaonyesha dhahiri kuwa anahofu na lile Kufuli la BASATA linaweza likamshukia kwa mara ya pili baada ya ya kunyamazishwa katika wimbo wa Shika Adabu yako ambao ulitoka kabla ya huu unaotamba kwa sasa.

Katika ukurasa wake wa instagram Hit maker huyo wa ‘Saka hela’ anayejulikana zaidi kwa mashairi ya hip hop ambayo mengi hujikuta akiwasema watu kwa kutumia mistari ya ubunifu aliweka wazi hofu yake  juu ya kufungiwa.

“Zimebaki siku kadhaa tu, Jumatatu Tarehe 11. Nitakua naachi wimbo wangu mpya. ‘Pale kati Patamu’ hii ngoma daaah mpaka napagawa yani. Shika iyo Tarehe na siku pale kati patamu sijui wataleta zengwe na hii?” alimalizia Nay wa Mitego kwa staili ya kuuliza.

Mgombea Urais wa Democrat, Hillary Clinton aanza kuchunguzwa
Video: Mwanamke aliyekolewa akiwa hai baada ya kusombwa na mafuriko kilomita 60