Msanii wa Bongo Flava, Nay Wa Mitego amemvaa mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba na kudai kuwa yeye ni mnunuaji mkuu wa tafiti, wasanii kwa lengo la kukisaidia chama chake.

Nay alimjibu January Makamba aliyepost ujumbe akionesha kushangaa tuhuma dhidi ya CCM kuwa imekuwa ikinunua wanasiasa, tafiti pamoja na wasanii kwa lengo la kuulaghai umma.

“Zitto kanunuliwa. Slaa kanunuliwa. Lipumba kanunuliwa. Twaweza imenunuliwa. Synovate imenunuliwa. Wasanii wamenunuliwa. Tuwe creative kidogo,” alindika January Makamba.

“Uongo? We ndo mnunuzi mkuu. Bro kama ubunifu ni hela basi we Master wa Ubunifu… @JMakamba Ongeza ubunifu bro,” alijibu Nay wa Mitego.

Alichokisema Roma Baada Ya BASATA Kuufungia Rasmi Wimbo Wake ‘Viva’
Simba Yanga ni ‘Afe Punda Mzigo Uende’