Wiki moja baada ya kundi kubwa la wakubwa wa mainstream Tanzania kunogesha uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM walipomnadi mgombea wao Dk. John Magufuli, Jumamosi hii ni zamu ya Chadema na ngome ya Ukawa kupewa shavu na safu inayoongozwa na wana hip hop.

Mkali wa hip hop toka Tanga anaefahamika zaidi kwa mashairi yake ya kupinga ufisadi, Roma Mkatoliki, ametajwa kuwa kati ya wasanii watakaoburudisha maelfu ya wananchi wanaotarajiwa kufurika katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam kusikiliza sera za vyama vinavyounda Ukawa.

Wengine ni Ney wa Mitego ambaye miaka mitatu iliyopita alisikika kwenye wimbo wake akiahidi kumpigia kampeni Lowassa endapo atagombea urais mwaka 2015, wazo ambalo wengi walilichukulia kama ndoto kwa kuwa wakati huo ndipo sakata la Richmond lilikuwa bado linatokota mitaani.

Ratiba iko pale pale… Tukutane Jangwani, #Mabadiliko2015

A photo posted by NayTrueboy (@naytrueboy) on

Mbali na wasanii hao, mwingine anaetarajiwa kuimba ni mgombea ubunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule aka Profesa Jay na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu amethibitisha uwepo wa wasanii hao katika tukio hilo na kuongeza kuwa wasanii wa filamu watakaokuwepo ni pamoja na Jackline Wolper, Aunt Ezekiel na Maimartha.

Mwalimu amewataka wananchi kuhudhuria kwa wingi ili kuielewa Ilani ya chama hicho.

Mwakyembe Amng’ang’ania Lowassa Kashfa Ya Richmond
Stars Yashindwa Kung’ara Dhidi Ya Libya