Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani imeendelea alfajiri ya leo kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja tofauti ambapo Indiana Pacers wameibuka na ushindi wa alama 98-95 dhidi ya Washington Wizards.

Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali kati ya timu zote mbili na kila moja ilikuwa imekamia kupata ushindi lakini bahati ikaangukia kwa Pacers.

Victor Oladipo alipachika alama 33, Bojan Bogdanovic akaongeza alama 20 zilizoisaidia Indiana Pacers kupata ushindi wa alama 98-95.

Myles Turner akaongeza alama 12 na 13 Rebounds ambazo ziliwasaidia kuongoza kwa alama 17 zaidi, lakini Indiana walimaliza mchezo wa nne kwa 2-2 baada ya kupoteza mara mbili.

Kwa upande wa Washington Bradley Beal amefunga alama 22 na kutoa pasi za mwisho 11 ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kufunga kwa upande wake.

Huu ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Washington kupoteza ikiwa ni mara ya kwanza hali hiyo kuwatokea msimu huu.

Beal msimu huu anaongoza kwa kupachika alama nyingi zaidi ndani ya timu ya Wizards kutokana kiwango anachoonesha katika kila mchezo.

Otto Porter Jr akaongeza alama 17 kwa upande wa Wizards ambazo hazikuwa na faida kutokana na kupoteza mch

Diwani mwingine ajiuzulu na kuhamia CCM
Waamuzi watanzania hatarini kufungiwa