Shindano la Mchezo wa Golf la kumuenzi aliyekuwa mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo “NBC Lugalo Patron Trophy” linatarajiwa kufanyika 27 Agosti 2022 katika viwanja vya Jeshi la ulinzi la wananchi Lugalo Dar es Salam.

Akizungumzia ujio wa shindano hilo mwenyekiti wa klabu Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luongo amesema,pia lengo la shindano hilo ni kumkaribisha mlezi mpya wa klabu ambaye ni mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda.

Naye kwa upande wake mwakilishi kutoka benki ya NBC ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo mkurugenzi wa wateja binafsi na wateja wadogo Ellibariki Masuke ameishukuru Klabu ya Lugalo golf kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo na amewaomba wadau na Watanzania wajitokeze kwa wingi katika shindano hilo.

Benki ya NBC imekabidhi vifaa vya mchezo huo ambavyo vitatumika katika shindano hilo,”NBC Lugalo Patron Trophy'” linarotarajiwa kufanyika 27 Agosti 2022, ambapo mgeni rasmi katika ufungaji wa shindano hilo anatarajiwa kuwa waziri wa utamaduni, sanaa na michezo mhe. Mohammed Mchengerwa.

Sekta binafsi zatakiwa kuwekeza kwenye Mifugo na Uvuvi.
Watafiti watakiwa kuwa msaada vivutio vya utalii