Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo ameomba radhi bungeni mjini Dodoma kwa kitendo kilichofanywa na askari polisi cha kuwadhibiti kwa kutumia nguvu kubwa watu wenye ulemavu Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kuwadhibiti watu hao na kusema kuwa wao kama Serikali wamelipokea jambo hilo na ameahidi kulifanyia kazi ili lisiweze kujirudia tena.

“Kwanza naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa, ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie,” amesema Nchemba.

Hata hivyo, watu hao wenye ulemavu mnamo tare 16 June 2017 walishambuliwa na jeshi la polisi Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwatawanya walipokuwa wamekusanyika kwaajili ya kutaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwasilisha malalamiko yao ya kuzuiliwa kuingia katikati ya jiji ili waweze kufanya shughuli zao.

 

Ndanda FC Waibuka Na Mbinu Mbadala
Ngonyani awatibua wapinzani bungeni, awapiga kijembe cha kula rambirambi