Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa baadhi ya wanasiasa wanaohubiri sakata la Lissu kupigwa risasi wanafanya siasa kwani ukweli ni kwamba bila serikali kiongozi huyo angekuwa amepoteza maisha.

Ameyasema hayo mkoani Singida, ambapo amedai kuwa bila jitihada za serikali huenda Mbunge huyo wa Singida Mashariki Tundu Lissu angekuwa amepoteza maisha kufuatia shambulio la kupigwa risasi akiwa mjini Dodoma.

“Lissu aliposhambuliwa daktari aliyekwenda kuokoa maisha yake yaani huduma ya kwanza ile ambayo isingefanyika Lissu angepoteza maisha yake ilifanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ambaye ni mteule wa Rais,”Hawa wanakuja wanaongea ongea juu ya Lissu hata hawatokei hapa Singida angekuwa mtu anayetokea Singida ilibidi aipongeze Serikali kwa kazi iliyofanya baada ya Lissu kushambuliwa,”amesema Nchemba

Hata hivyo, Nchemba amewataka wanasiasa kutotumia tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na kufanyia siasa waache mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume na maadili.

Penzi la Diamond na Zari latia nanga, Zari aanika madudu ya Diamond
Video: Lissu acharuka mauaji Chadema, Wananchi wampasha DC mbele ya RC