Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa serikali imejipanga vizuri ili kuweza kuondoa msongamano wa mahabusu gerezani.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kuwaweka mahabusu watu wengi ni kuisababishia hasara kubwa serikali.

Amesema kuwa kufunga watu sio jambo la kujivunia hivyo taasisi za kiroho zinatakiwa kufanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii.

“Hicho ni kitu ambacho tumekipa kipaumbele mkubwa, mimi sifurahii sana kujaa kwa magereza, nataka tupunguze yote haya,”amesema Waziri Nchemba.

Wafanyakazi wakatwa mishahara kuchangia uchaguzi
Chameleone awatimua kwa panga waombolezaji msiba wa Radio