Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewashangaa vyama vya upinzani kwa kuweka wagombea katika uchaguzi mdogo wa madiwani nchini kwani kwasasa ilani inayofanya kazi ni ya CCM na kwamba hao wagombea wao wataenda kutekeleza ilani gani.

Ameyasema hayo wakati akiwa katika kata ya Siuyu Jimbo la Singida Mashariki wilaya ya Ikungi alipokuwa akifungua kampeni za mgombea Udiwani kupitia tiketi ya CCM baada ya diwani Gerald Mahami wa CHADEMA kuvuliwa uongozi kutokana na kutoshiriki vikao vya baraza la madiwani la halmashauri ya Ikungi.

Amesema kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 kila mtu alileta mgombea wake akiamini atashinda na baadae mgombea wa CCM Rais Dkt. Johm Magufuli alishinda na ilani ya CCM ndiyo inayotekelezwa hivyo haoni haja ya wapinzani kusimamisha mgombea.

Aidha, ameongeza kuwa watu kuwa na vyama vingine si kosa na wala kuwa na kadi ya chama kingine si lazima upigie chama chako bali upige kura kwa diwani ambaye ilani yake ndio inatekelezwa kwa wakati huo.

“Tulipokuwa kwenye uchaguzi Mkuu kila chama kilikua na sera zake na kila mtu alikuwa na wagombea wake huku kila chama kikiamini kwamba kitashinda ngazi zote.  Sasa kwenye uchaguzi huu mdogo hatunadi ilani kwani inayotumika ni hii ya CCM,”amesema Nchemba

Video: Deontay Wilder atamba kumpiga Anthony Joshua
Trump atoa onyo kali kwa Rais wa Korea Kaskazini