Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa kwa sasa viongozi wa umma wakiwamo mawaziri, hawana ubunifu kwa sababu ya hofu waliyo nayo.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2019/20.

“Leo hii ukienda kila mahali wafanyabiashara wana hofu. Ukienda kwenye taasisi kuna hofu, mawaziri wana hofu, makatibu wakuu wana hofu, maendeleo yanaletwa na vitu vingi bila viongozi kujiamini hawawezi kuwa waaminifu,” amesema Lema.

Aidha, amesema kuwa katika maeneo mengine wakuu wa mikoa wanaonekana kuwa na nguvu kuliko hata mawaziri, kitu ambacho amesema si sawa.

pia amegusia suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji na kusema polisi wamekuwa wakilifanya jambo hilo kama sinema.

 

Rostam Azizi atinga Ikulu kuonana na JPM
Gutteres azitaka Israel na Hamas kusitisha mapigano

Comments

comments