Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa haiingii akilini kwa serikali kuagiza malighafi za kujengea reli nchini, wakati tuna makaa ya mawe na chuma wilayani Ludewa, ambayo mpaka sasa hayajaanza kuchimbwa.

Amesema kuwa serikali ingechukua hatua katika kutengeneza kiwanda cha chuma kutokana na madini ya chuma yaliyopo Ludewa, serikali isingeingia gharama ya kuagiza malighafi za ujenzi wa reli nje, na pia ingeweza kupata kipato kwa kuuza kwa nchi jirani kama Kenya na Zambia, ambako nako kuna ujenzi wa reli unaendelea.

“Kweli inaingia akilini tuna chuma na makaa ya mawe yamejaa pale Ludewa, tunampa mkandarasi kazi ya kujenga reli, vyuma vinatoka Uturuki, India, China kweli Mh. Spika!!? Kenya nao wanajenga reli tungeweza kuwauzia,”amesema Zitto

Hata hivyo, Zitto Kabwe amesema kuwa nchi inatia aibu kuagiza mafuta kutoka nje na kuibua mgogoro mkubwa kuhusu bidhaa hiyo, wakati nchi ina rasilimali za kutosha za kutengeneza mafuta, ila haijaweka mikakati wala mipango yoyote kukuza sekta hiyo.

Hizi hapa sababu 7 za kutumia chai ya kahawa
Alikiba aipa tano 'Hapa Kazi tu' ya JPM