Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema tayari nchi imekumbwa na wimbi la tatu la ugonjwa wa COVID-19 na kwamba wagonjwa wa ugonjwa huo wapo ambapo amewaomba viongozi wa dini kuwakumbusha  waumini kuhusu umuhimu wa kujikinga na ugonjwa huo.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 25, 2021, mkoani Dar es Salaam, alipokutana na kuzungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini (TEC).

Sasa hivi kuna wimbi la tatu la Corona, ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana katika hili wimbi la tatu, kama mnakumbuka siku nimetembelea hospitali ya Mwananyamala daktari aliniambia kuna wodi ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, alisema Rais Samia.

”Daktari nikamuambia ni COVID-19 akasema ndiyo, wakati wapiga picha wangu walikuwa wamekwishatangulia nikawaambia ninyi ebu tokeni haraka huko, hili jambo lipo, tunawaomba sana viongozi wa dini mliseme hili kwa waumini ili tujiepushe na vifo vya makundi”amesema Rais Samia.

Aliyemuua George Floyd apigwa miaka 22 jela, Jaji amuongeza lingine
Mbowe, wenzake wafutiwa kesi