Lesotho na Comoro ndio nchi pekee kati ya nchi 54 za bara la Afrika ambazo hazijakumbwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Imeelezwa kuwa takriban watu 9,500 wameambukizwa barani Afrika kote, 400 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19, na wengine 900 wamepona.

Sao Tome and Principe imekuwa nchi ya 52 barani Afrika kutangaza maambukizi ya virusi vya corona. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Jorge Bom Jesus amethibitisha kuwa watu wanne wameambukizwa baada ya kufanyiwa vipimo.

Wakati huo huo shirika la afya duniani WHO limetoa wito wa kufanyika juhudi za pamoja ili kupambana na janga la corona. Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi zote zinapaswa kuwa na mkakati wa pamoja.

Said Ndemla kumalizia mkataba Simba SC
CORONA: Awaua jirani zake kisa walimpigia kelele wakati kuna amri ya kubaki nyumbani