Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amefanya ziara ya kushtukiza katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) na kufanya ukaguzi wa vibali vya wafanyakazi na maabara na kubaini kuwa baadhi ya walimu huishi nchini bila Ubora wa vibali.

Ziara hiyo imefanyika leo, 20 Februari 2018 akiwa ameambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala, Mkuu wa Ithibati na Udhibiti ubora wa vyuo Vikuu Tanzania.

Ndalichako amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwemo walimu wa chuo hicho kuajiriwa sehemu zaidi ya moja na kuishi nchini bila vibali.

Amesema wapo walioingia nchini kama wanafunzi lakini baada ya muda wakaajiriwa kama wafanyakazi hii kwa sheria za nchi haikubaliki amesema Profesa Ndalichako.

Aidha, Ndalichako ameshangazwa na wanachuo wa mwaka wa kwanza kudai kutofahamu viongozi wakuu wa chuo licha ya kufanyiwa utambulisho leo.

Mambosasa aagiza vigogo 7 wa Chadema kuwekwa chini ya ulinzi
Mtumishi TRA mbaroni kwa ulawiti