Jeshi la Polisi linamshikilia Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Mgalla Mashaka kwa tuhuma za kushindwa kukarabati Shule ya Sekondari Kigoma.

Mhandisi Mgalla amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo, mabweni, maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika.

Aidha, baada ya Mhandisi huyo kushikiliwa na Jeshi la Polisi, Prof. Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea.

Hata hivyo, Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo kama ilivyopangwa.

 

 

Kitabu chenye utata kuhusu Rais Trump kuingia sokoni
Magazeti ya Tanzania leo Januari 5, 2018