Waziri wa elimu sayansi teknolojia na mafunzo ya ufundi, Joyce Ndalichako ametoa ufafanuzi juu ya utolewaji wa adhabu ya viboko kwa wanafunzi na kusema kuwa mwanafunzi anatakiwa kuchapwa viboko visivyozidi vinne.

Amesema kuwa sheria lazima ichukue mkondo wake kwa walimu watakaokiuka sheria hiyo kwani kumekuwa na matukio ya kusikitisha yanayohusha walimu kuchapa wanafunzi viboko huku akitaja tukio la Kegera la mwalimu kumchapa hadi kumsababishia mwanafunzi kifo, na nyingine juu ya mwalimu kumchapa mwanafunzi hadi kumvunja mgongo.

”Adhabu ya viboko vinavyotakiwa kufanyika ni viboko visivyozidi vinne lakini ile adhabu inapotolewa mkuu wa shule ndiye anayetakiwa kuchagua ni mwalimu yupi anatakiwa kutoa adhabu hiyo” amesema Nsdalichako.

Aidha amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya na kutoa onyo kali kwa wale walimu wachache wanaoichafua tasnia ya ualimu.

”Tunapokuwa tunafanya vitu kinyume na sheria , sheria itachuka mkondo wake na baadae mtasema hamtetewi hakuna mtu atakayekuwa anamtetea mtu anayevunja sheria” amesema Ndalichako.

Ameongezea kwa kuwasihi walimu kuendelea kufanya kazi vizuri kwa kufuata sheria kanuni na utaratibu ikiwa ni pamoja na utoaji adhabu pale inapobidi kutoa adhabu.

Serikali ya Mali yajiuzulu, umma waikataa
Video: Fahamu nyoka hatari wenye sumu kali zaidi duniani