Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, ametangaza ratiba ya mitihani ya kidato cha nne, kidato cha kwanza na darasa la saba ambayo itamalizika Disemba 11.

Waziri Ndalichako amebainisha hayo leo Juni 17, 2020, Jijini Dodoma, na kusisitiza kuwa shule zizingatie mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya juu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Corona kama ambavyo vyuo vimefanya kwani hadi sasa hakuna mwanafunzi aliyepata Corona.

“Darasa la 7 wataanza mitihani yao Oktoba 7-8, Kidato cha 2 wataanza mitihani yao Novemba 9 hadi 20, wanaomaliza Kidato cha Nne na wa kujitegemea na wale wanaofanya mitihani ya maarifa, wataanza Novemba 23 hadi  Disemba 11, na Darasa la Nne wataanza Novemba 25 – 26, 2020”.

Kwa upande wa malipo ya ada za shule, ametoa wito kwa wamiliki wa shule kutumia busara na kufanya maridhiano na wazazi ili wanafunzi waendelee na masomo.

“kuhusu suala la Ada Tanzania tuwe na moyo wa kupendana hili suala busara na maridhiano kati ya shule ba wazazi wito wale wazazi ambao walikuwa hawajakamilisha muhula wa kwanza wakamilishe, si vizuri kumkataa mtoto kisa hajamaliza Ada waweke makubaliano”. Amesema Ndalichako.

Kuhusu muda wa masomo amesema “Shule Inapofunguliwa wanafunzi watasoma mpaka December 18 mwaka huu ndipo watafunga shule na muda wa masomo uongezwe kwa Saa mbili zaidi ili kufidia muda wa ziada.”

Ruvu Shooting waitumia salamu KMC FC
Magufuli achukua fomu ya Urais, kutafuta wadhamini siku 17