Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako ameingilia kati sakata la mwanafunzi  shule ya msingi Kibeta Mkoani Kagera wa darasa la tano, Sperius Eradius (13) aliyefariki dunia kwa kupigwa bakora na mwalimu wake kwa kutuhuma ya kuiba pochi ya mwalimu juzi, Jumatatu, Agosti 27, 2018.

Prof. Ndalichako amesema kila mwaka Serikali inatoa hela kiasi cha Bilioni 20 katika mashule hela hizo hazitolewi kwa ajili ya watoto kupata matishio wala wakapoteze maisha yao, hivyo amesema kwa mwalimu yeyote atakaye onekana kuwatishia watoto pindi wakiwa mashuleni watakamatwa na kushughulikiwa vikali na Serikali.

Amesema bahati mbaya iliyotokea kwa mwalimu huyo isitafsiriwe kama shule sio sehemu salama kwa watoto kujifunzia kwani hata serikali haikumtuma mwalimu yule kufanya kitendo kile alichokifanya dhidi ya marehemu Sperius Eradius.

”Bahati mbaya ambayo imetokea kwa hiyo bahati mbaya hiyo kwa namna yeyote ile isije ikatafsiriwa kama shule sio mahali salama na kwa yeyote yule ambaye anahatarisha usalama wa watoto shuleni serikali itamshughulikia kwa nguvu zote sababu serikali inaamini kwamba elimu ni nyenzo muhimu kwa watoto ndio maana kila mwezi rais anatoa bilioni 20, hawatoi hela ili watoto wakapate matishio au wakapoteze maisha shuleni” amesema Ndalichako.

Amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa mwalimu atakayetishia amani kwa watoto kwani Serikali inataka watoto wote Tanzania wapate maarifa na ujuzi kwa amani ili waweze kuchangia maendeleo katika nchi.

Aidha amewaomba watanzani wawe na amani na utulivu katika kipindi hiki ambacho serikali inashughulikia suala hilo.

Kocha wa Stars Awatema wachezaji wa Simba
Kenya Yajitoa kuandaa michuano ya CECAFA 2018