Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako, amepiga marufuku vyuo na shule zenye wanafunzi wa kidato cha sita zitakazofunguliwa Juni 1, kuzgiza wanafunzi kwenda shule na Tangawizi, malimao, na spriti.

Amesema sio kila chuo au shule kinatakiwa kuutoa mwongozo wake, ikiwemo kuwataka wanafunzi kwenda na spriti, tagawizi na vitu vingine, badala yake wanatakiwa kufuata mwongozo wa Wizira ya Afya.

Onyo hilo limetolewa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo pia ameonya wanafunzi kuanza kudaiwa ada wakati walikuwa wameshalipa ada kabla ya kufunga shule, kwa hiyo walikuwa nyumbani kwa sababu kulikuwa na changamoto ya ugonjwa.

“Watu waache kutumia Corona kama kitega uchumi kwa kuanza kuagiza fedha za ziada, Wanafunzi walikuwa wameishalipa ada kabla ya kufunga shule, kwa hiyo walikwenda nyumbani kwa sababu kulikuwa na changamoto ya ugonjwa,” amesema Ndalichako

Amesema Wizara ya afya imesisitiza na kushauri wazazi kuwapatia watoto wao barakoa ambazo zimeshonwa kwa kitambaa ambazo mwanafunzi anaweza akafua akapiga pasi.

Aidha amesisitiza wanafunzi wanapoenda shuleni wazingatie umbali kati ya mtu na mtu, wajiepushe na misongamano iwe ni katika majadiliano, kwenye mabweni na wakati wa kula, ni muhimu wakazingatia taratibu ambazo zinatolewa na Wizara ya Afya na watahakikisha taasisi zote zinaupata mwongozo huo.

Kikwete athibitisha usalama Hosteli zilizotumika karantini UDSM
Ianis Hagi kubaki Ibrox Stadium

Comments

comments