Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom 2016/2017 limefunguliwa kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku macho ya wanamichezo wengi nchini yakiwa katika uwanja wa Taifa ambapo Simba SC ilikuwa mwenyeji wa Ndanda ya Mtwara.

Mchezo huo umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Ndanda, na hivyo kuiwezesha Simba kuondoka na alama zote tatu za mchezo huo.

Magoli ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Laudit Mavugo dk. 17, Fredrick Blagnon dk. 74 na Shiza Kichuya katika dakika ya 79 huku goli pekee la Ndanda likifungwa na Omary Mponda dk. 35

Mchezo unaofuatia kwa Simba inataraji kuwa mgeni dhidi ya JKT Ruvu, mchezo ambao utapigwa kupigwa Agosti, 27.

Tume Ya Mipango Yakamilisha Mafunzo Ya Wataalamu Usimamizi Miradi Ya Umma
Wizara ya Elimu: Mabilioni yaandaa hafla hewa, Jengo hewa Dodoma