Baada ya Toto kukufungwa 1-0 katika mchezo wa mwanzoni mwa juma hili dhidi ya Ndanda FC, kocha mkuu wa Toto Africans Rogasian Kaijage ametangaza kuachia ngazi nafasi ya kuifundisha timu hiyo ya jijini Mwanza.

“Ni kweli nimefanya uamuzi huo toka jumatatu, leo ndiyo nilikuwa napeleka barua kwa uongozi ili kuwaambia rasmi. Nilitoa taarifa ya awali kwa message lakini ni kweli kwamba mimi nimeiacha Toto. Ni suala refu lakini kimsingi Tanzania watu huwa tunafanya vitu bila kujua mwelekeo wake, katika mpira tuna tatizo la uchungu wa matokeo lakini si uchungu wa kuiandaa timu au kuandaa matokeo.”

“Naweza kusema nilikuwa najitolea kuwasaidia lakini kwa sababu imetokea matokeo yamekuwa sio mazuri sasa uchungu wa matokeo kwa ambao hawajui matatizo yaliyomo ndio walitaka kunivamia na kutaka kunipiga wakisema niwaachie timu yao. Sasa kama nawasaidia halafu watu wanataka timu yao kwa sababu ya matokeo kwa nini nisiwaachie.” Alisema Kaijage

Dogo Janja atangaza ndoa, Madee aiita dharau
ZFA Yawakaribisha Young Africans Uwanja Wa Amaan