Ndege ya abiria iliyokuwa imebeba jumla ya watu 62 leo imeanguka wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege ulio katika mji wa Rostov-on-Dov nchini Urusi.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 inayomilikiwa na kampuni la FlyDubai ilikuwa ikisafiri kutoka Dubai, ilikuwa imebeba abiria 55 na wahudumu 7 na hakuna hata mmoja aliyesalimika.

Ndege ilivyoanguka

Taarifa zilizotolewa na Waziri wa Masuala ya Dharura nchini Urusi, Vladimir Puchkov imeeleza kuwa chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo kunaweza kuwa hali mbaya ya hewa na kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua mara mbili bila mafanikio kabla ya kuanguka.

Ndege hiyo ilikuwa inatarajiwa kutua majira ya saa 7:20 usiku kwa majira ya huko lakini ilianguka majira ya saa 9:50 usiku.

P Square: Paul amuomba msamaha Peter, maneno yake ya kubembeleza yazaa hili
NEC yatangaza kusimamia uchaguzi wa Zanzibar ‘Kijitoupele’