Safari ya ndege ndefu zaidi duniani imeanza nchini Uingereza baada ya majaribio ya awali kushindikana  dakika za mwisho.

Ndege hiyo inayojulikana kwa jina la Airlander 10, ambayo pia ni meli  inauwezo wa kufanya safari zake majini kama meli zingine, imezinduliwa kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Cardington huko Bedfordshire nchini Uingereza.

Ndege hiyo inakadiriwa kuwa na gharama ya pauni milioni 25 na ina urefu wa mita 93, urefu wa mita 15 zaidi ya ndege yoyote kubwa ya abiria duniani.Ndege hiy0 kwa mara ya kwanza ilitengenezwa  na serikali ya Marekani kwaajiri ya kufanya ujasusi lakini mradi huo ulishindikana kutokana na ukosefu wa fedha.

Kampuni ya uingereza ya Hybrid Air Vehicles (HAV) ilizindua kampeni hiyo  na kufanikisha mradi huo.

Ndege hiyo ina uwezo wa kukaa angani kwa takriban siku tano na itatumiwa katika masuala ya Kiserikali yakiwemo ujasusi, mawasiliano, kusafirisha misaada na hata abiria

Raila Odinga: Magufuli amesema hajakataza mikutano kwa walioshindwa uchaguzi
Tume Ya Mipango Yakamilisha Mafunzo Ya Wataalamu Usimamizi Miradi Ya Umma