Ndege nyingine ya kampuni ya Boeing imelazimika kutua kwa dharura baada ya rubani kubaini kuwa kuna tatizo kwenye mfumo wa injini.

Ndege hiyo namaba 8701ya Shirika la Ndege la Southwest imeripotiwa kushindwa kuendelea na safari yake kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa orlando kwenda Victorville, California nchini Marekani.

Shirika hilo  la ndege limeeleza kuwa ndege hiyo ililazimika kutua kwa dharura Jumanne wiki hii, kwa muda mfupi kabla ya kuendelea na safari yake kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo madogo.

“Wafanyakazi wa ndege walifuata protokali na kufanikiwa kutua tena kwenye uwanja wa ndege,” limeeleza shirika hilo kwenye taarifa yake.

Machi 13, Marekani iliamuru ndege zote za Boeing 737 Max kutoruka, kufuatia kuanguka kwa ndege mbili za aina hiyo, Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu.

Bado haijafahamika wazi kuwa ndege hiyo ambayo haikuwa na abiria ilikumbwa na tatizo kama la ndege hizo mbili zilizoanguka au ni tofauti.

Video: Filamu ya "US" ya Lupita Nyong'o yaweka rekodi
Video: Nassari anapaswa kulipa fidia- Wakili Manyama