Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe ameomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) waliokuwa wasafiri kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg Afrika Kusini kuelekea jijini Dar es salaam nchinj Tanzania kufuatia ndege hiyo kushindwa kufanya safari hiyo kama ilivyopangwa.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo serikali imepokea kutoka kwa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, ndege hiyo imezuiliwa kwa amri ya mahakama ya Gauteng ya jijini Johannesburg.

Aidha, taarifa hiyo ya wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Leonard Chamuriho imesema kuwa serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa inafuatilia suala hilo ili ndege hiyo iachiwe mara moja na kuendelea na safari zake kama kawaida.

 

Video: Kaka yake Lissu afunguka, 'Hii kesi sio ya hovyo'
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 24, 2019