Ndege ya Bangladeshi iliyokuwa imebeba abiria 67,  ambapo 32 kutoka Bangladeshi huku 33 kutoka Napel na abiria mmoja kutoka China imepata ajali na kulipuka papohapo wakati ikiwa inatua katika uwanja wa ndege wa Nepali na kusababisha vifo vya watu 50.

Ndege hiyo inayoendeshwa na shirika la ndege la Marekani la Bangla Airlines, ilikuwa kwenye safari ikitoka Dhaka ilipokuwa inatua ilijikuta ikigonga uzio wa uwanja huo wa ndege na kulipuka.

Hayo yamesemwa na Raj Kumar Chettri ambaye ni meneja mkuu wa uwanja huo wa ndege.

Msemaji wa jeshi la polisi Nepali, Gokul Bhandari amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya mlipuko wa ndege na amesema

‘’Mpaka sasa tumepata miili ya watu 50 ambao wamefariki dunia na huku wengine 9 wakiwa hawajulikani walipo, Hata hivyo bado  jeshi la polisi linaendelea kuokoa watu wengine kufuatia mlipuko huo wa ndege aina ya Bombardier Q400’’.

Hata hivyo taarifa zilizotolewa na tovuti ya Flightradar24.com zimeonesha kuwa ndege hiyo imefanya kazi kwa miaka 17.

 

Kubenea akanusha kufukuzwa ofisini
Macron na Modi wazindua mfumo wa umeme jua Delhi