Ndege ya abiria aina ya Boeing 737 jana ilitua ghafla ikikita ardhini na kutereza hadi mtoni kufuatia mtetemo mkali wa radi katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Jumla ya watu 143 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, ikiwa ni abiria 136 na wahudumu saba wameripotiwa kuwa katika taharuki kubwa.  Ingawa hakuna aliyepata majeraha makubwa lakini watu 21 walipewa matibabu kwa majeraha madogo, kwa mujibu wa CNN.

Ndege hiyo inayofanya kazi chini ya Shirika la Miami Air Internation ilikuwa ikisafiri kutoka Guantanamo Bay nchini Cuba kuelekea kwenye eneo la jeshi la Jacksonville, ambapo ilitua kwa kishindo na baadaye kutereza hadi kwenye mto wa St. John.

Abiria aliyejitambulisha kwa jina la Cheryl Bormann ameiambia CNN kuwa wakati ndege inatua kwa kishindo watu walipiga kelele.

“Ndege ilitua kwa kishindo na tulisikia kama inakita ardhi na kuyumba, ilikuwa wazi kuwa rubaini ameshindwa kuidhibiti, ikatikisika tena,” alisema Bormann.

“Tulikuwa ndani ya maji. Hatukuweza kufahamu tuko wapi, hatukujua ilikuwa ndani ya mto au ndani ya bahari na kukaanza kusikia harufu ya mafuta ya ndege kama yamevuja ndani ya maji,” aliongeza.

Captain Michael Connor wa NAS Jacsonville ameeleza kuwa hali ingekuwa mbaya zaidi huku akielezea namna ilivyotua kama ‘muujiza’.

Ferooz: Wanatumia uchawi kumbomoa msanii watengeneze brand zao
Mose Fan Fan wa 'Papa lolo' afariki dunia

Comments

comments