Rais Dkt. John Magufuli leo Jumapili Julai 08, 2018 ataongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania.

Hii ni ndege ya 4 kuwasili nchini Tanzania kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania chini ya utawala wa awamu ya tano wa Rais John Pombe Magufuli katika harakati ya kuliwezesha Shirika la Ndege Tanzania, ATCL.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana leo ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.

CUF yatangaza kusitisha kushiriki uchaguzi mdogo wa marudio
Video: Mwigulu, 'Niliomba ubunge na si uwaziri', Dege la JPM kutua leo

Comments

comments