Watu 16 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya ndege ya jeshi la Marekani waliyokuwa wakisafiri nayo kuanguka kusini mwa jimbo la Mississippi, Jumatatu jioni.

Ndege hiyo ilianguka na kushika moto katika eneo la LeFlore, umbali wa kilometa 160 kutoka katika jiji la Jackson.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa idara ya dharura ya ya Leflore, Fred Randle abiria wote walikuwa wanajeshi na hakuna hata mmoja aliyesalimika ndani ya ndege hiyo.

Gavana wa jimbo la Mississippi, Phil Bryant amesema kuwa tukio hilo ni janga kubwa kwani askari hao walikuwa kazini wakijitolea maisha yao kila siku kuhakikisha wananchi wanafaidi uhuru wao kwa amani.

“Watu wetu wanaume na wanawake walikuwa kwenye sare zao wakijitolea maisha yao kila siku kulinda uhuru wetu,” alisema Gavana Bryant.

Bado hakuna maelezo rasmi ya kina kutoka kwa vyombo vya usalama kuhusu tukio hilo la kuanguka kwa ndege ya jeshi ikiwa ni pamoja na chanzo cha ajali hiyo.

Video: Ngeleja ajaribu kukwepa Keko, Majipu sasa yanajitumbua yenyewe - JPM
JPM amteua Prof.Luoga kuwa mwenyekiti TRA