Rubani wa ndege ya jeshi la Nigeria amefariki baada ya ndege aliyokuwa anaiendesha kuanguka wakati wa mazoezi kwa ajili ya maonesho katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya miaka 58 ya uhuru wa taifa hilo.

 Jeshi la Ulinzi la Nigeria limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa ndani ya ndege hiyo kulikuwa na marubani watatu ambapo kati ya hao walifanikiwa kuwaokoa marubani wawili tu.

Jeshi hilo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari limesema kuwa uchunguzi umeanza kufanyika ili kubaini sababu halisi za kuanguka kwa ndege hiyo.

“Baada ya kuanguka, tuliweza kuwaokoa marubani watatu kutoka kwenye ndege hiyo ambayo ilianguka katika eneo la Katamkpe Hill. Tunasikitika kueleza kuwa mmoja kati yao alifariki muda mfupi baadaye. Tunashukuru kuwa hakuna raia aliyeathiriwa na ajali hiyo,” imeeleza.

Kama ilivyo kwa nchi nyingine, Nigeria huadhimisha kumbukumbu ya siku ya uhuru kwa kufanya maonesho ya ndege za kivita pamoja na gwaride maalum la majeshi.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 30, 2018
Akaunti milioni 50 za Facebook zadukuliwa, yammiliki pia