Shirika la Ndege la Usafriri wa anga, Precision Air limethibitisha taarifa za ndege zake mbili kuwa zimeshindwa kufanya safari zake kama kawaida baada ya ndege moja kupata hitilafu na nyingine kulazimika kutua kwa dharura.

Taarifa ya shirika hilo imesema, moja ya ndege zake ilipata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa safari na nyingine ililazimika kutua kwa dharura.

Kutua kwa dharula kwa ndege hiyo, kunatokana na Ndege hiyo kugonga kiumbe aina ya ndege wakati ikiruka kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Novemba 6, 2022, Ndege ya Shirika hilo aina ya ATR 42-500 yenye namba PW 494 iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kupitia Bukoba ikiwa na watu 43 ilipata ajali na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 26.

Serikali yajivunia mafanikio kupitia PEPFAR
Aliyekuwa mke wa Manara aeleza uhusiano wake na Harmonize