watu 97 wamefariki dunia na wawili wameokolewa wakiwa hai baada ya ndege kuanguka jana katika makazi ya watu Kusini mwa jiji la Karachi nchini Pakistan.

Kwa mujibu wa wizara ya Afya ya Jimbo la Sindh, miili ya abiria na wahudumu wa ndege hiyo aina ya Airbus A320 ya Shirika la Kimataifa la Pakistan imepatikana na zoezi la uokoaji limehitimishwa asubuhi ya leo.

Imeelezwa kuwa muda mchache kabla ajali haijatokea, Rubani aliripoti matatizo ya kiufundi lakini bado chanzo kamili cha ajali bado hakijafahamika.

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Lahore na ilitakiwa kutua jijini Karachi kabla ya kupotea kwenye ramani.

Uimara huduma za afya wapunguza 30% ya wagonjwa wa Fistula Tanzania
Rais wa Zambia afungua mpaka na Tanzania