Ndege ndogo aina ya Cessna 172, jana  iligonga jengo lililoko katika Manispaa ya Anchorage, Alaska nchini Marekani na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Kwa mujibu wa ripoti ya FBI kuhusu tukio hilo, rubani aliyekuwa anaiendesha ndege hiyo aliyefahamika kwa jina la Doug Demarest mwenye umri wa miaka 42 alifariki. FBI ambayo inachunguza tukio hilo imeeleza kuwa rubani huyo aliirusha ndege hiyo bila kibali.
Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la kiraia linalosaidia kufanya ukaguzi wa usalama angani, utafutaji na uokoaji katika majanga mbalimbali.