Ndege iliyokuwa imebeba abiria 71 pamoja na mhudumu imeanguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa mjini moscow nchini Urusi.

Ndege hiyo ya shirika la Saratov ya An-148, ilikuwa safarini kwenda mji wa Orsk wakati ilipoteza mawasiliano.

Maafisa wa huduma dharura wameviambia vyombo vya habari kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na Argunovo kilomita 80 kusini mashariki mwa Moscow na hakuna uwezekano wa kuwapata manusura.

Kulingana na shirika lingine na habari ndege hiyo ilipotea kutoka mitambo ya rada dakika mbili baada ya kuondoka uwanja wa Domodedovo.

Mwita aacha neno baada ya akiungana na wananchi kupima Kisukari na Presha
Korea Kusini yaweka masharti kuhusu mwaliko wa Kim Jong-un