Ndege mbili za kivita za China aina ya Sukhou Su – 30, zimedaiwa kuzuia bila kufuata utaratibu ndege ya kivita ya Marekani iliyokuwa angani katika pwani ya China.

Afisa mmoja wa Marekani ameiambia CNN kuwa ndege moja kati ya hizo mbili ilifanya uzuiaji mbaya ikipita umbali wa mita 45 tu juu ya ndege ya Marekani huku ukijigeuza juu chini.

Marekani imedai kuwa ndege yake ilikuwa kwenye oparesheni maalum katika pwani ya China kwa lengo la kutaka kubaini jaribio la Korea Kaskazini la makombora ya kinyuklia.

“Kuzuia ndege ya Marekani kulikofanywa Jumatanu hakukuwa kwa kiueledi kwa sababu ya namna ulivyofanywa na rubani wa ndege ya China, vilevile mwendo kasi na ukaribu wa ndege zote mbili kwa ndege ya Marekani, Msemaji wa jeshi la anga la Marekani, Col Hodge aliiambia CNN.

Aliongeza kuwa suala hilo limewasilishwa kwa China kwa njia za kidiplomasia na njia za mawasiliano ya kijeshi na kwamba uchunguzi wa kijeshi unaendelea.

China haijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo, ingawa imekuwa ikiilaumu Marekani na kuitaka kupunguza hatua za ulinzi (patrol) katika eneo la pwani yake.

Simba yazifuata pointi tatu za ubingwa FIFA
China yaionya Marekani kutumia anga lake