Jeshi la Wanaanchi Tanzania (JWTZ) limejipanga kurusha angani ndege zake za kivita katika anga la Dar es Salaam, Septemba 1 mweaka huu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya kuanzishwa kwake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda amewataka wananchi kutokuwa na hofu wanaposikia ngurumo za ndege hizo bali wafurahie kwani ni ndege zao.

“Mnaposikia milio ya ndege zetu mbalimbali, mfurahie kwa sababu hizo ni ndege za wananchi. Usisikie muungurumo ukashtuka. Hakuna jambo lolote lile zaidi ya kuonesha vifaa vyetu na jinsi ambavyo wanajeshi wetu kwa miaka 52 wamaeendelea kuwa imara na vifaa vizuri,” amesema Makonda.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa wamewataka wananchi waliojipanga katika vikundi mbalimbali kuripoti kwa wakuu wao wa wilaya kujiandikisha ili waweze kushiriki pamoja na Jeshi hilo katika zoezi la usafi jijini humo.

Amewataka wakazi wa mkoa huo pia kujitokeza kuchangia damu katika vituo mbalimbali ambavyo vimeanishwa ili kuunga mkono juhudi za uchangiaji damu zitakazofanywa na wanajeshi wa JWTZ.

“Hii ni sehemu ya amani, tufanye usafi kwa amani. Tujitolee damu zetu kwa amani na mwisho wa siku tuwaenzi na kuwapongeza wanajeshi wetu kwa kazi kubwa wanayoifanya,” Makonda ameeleza.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa aliendelea kutoa onyo kwa watu watakaotaka kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku ya oparesheni UKUTA akiwataka kutii sheria.

AS Roma Waonyesha Nia Kwa Jack Wilshere, Lakini Waomba Msaada
Lowassa aandika Waraka kuhusu Ukuta, aeleza chanzo cha kukutana na Magufuli