Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, imetuma ndege mbili za kijeshi kupambana na waasi wa kundi la M23 wanaosonga mbele eneo la mashariki mwa nchi hiyo kuelekea mji wa kimkakati wa Goma.

Taarifa kutoka eneo hilo zinasema, vifaru vya jeshi na ndege mbili za kivita vimeyalenga maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji mdogo wa Kibumba, umbali wa kiasi kilometa 20 kutoka mji wa Goma.

Ndege ya Royal Air Force CH-47 Chinook ikiruka na Ndege mbili za USMC CH-53 Sea Stallions wakati wa mazoezi. Picha ya Wikimedia.

Hatua hizo za kijeshi zinafuatia juhudi za waasi wa M23 kuufikia mji wa Goma na kuzusha hofu ya kushambuliwa kwa mji huo.

Wakaazi wa maeneo ambako mapambano ni makali wamesema wapiganaji wa M23 wameanza kuelekea kwenye kitongoji cha Masisi kilicho magharibi mwa jimbo la Kivu Kaskazini wakiiacha ngome yao karibu na mpaka wa Uganda na Rwanda.

Ajali ya Basi yauwa 20, wamo watoto 11
Habari Picha: Waziri Mkuu ziarani Ruangwa