Ndege zisizo kuwa rubani zinatarajiwa kuanza kutoa huduma za kiafya hapa nchini mwanzoni mwa mwaka 2017, ili kurahisha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo mbalimbali ya nchi ambayo hayafikiki kirahisi.

Aidha lengo kubwa la Ndege hizo ni kusafirisha damu na vifaa mbalimbali na madawa kwenye kliniki za afya ili kupunguza usumbufu uliokuwa ukijitokeza hapo awali.

Ndege hizo zitakuwa chini ya Ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza(Dfid), ambapo halijasema litawekeza pesa kiasi gani katika mradi huo na kwa muda gani hapa Tanzania.

“Uvumbuzi huu wa kisasa unahakikisha tunafikia matokeo bora kwa ajili ya watu masikini zaidi duniani na kutoa huduma bora kutokana na pesa zinazotolewa na walipakodi Waingereza ,”amesema Katibu Mkuu wa Shirika hilo Priti Patel.

Mapema mwaka huu, Tanzania pia iliidhinisha kisheria matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani katika Mbuga ya wanyama ya Tarangire kama sehemu ya juhudi za kuzuia uwindaji haramu wa wanyamapori.

Lukuvi kula sahani moja na vigogo wanaomiliki majengo nchini
Video: Majaliwa ahimiza kilimo, 'wanaotaka fedha wataipata shambani'