Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya.
Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja.
Hata hivyo Ndemla atarejea nchini kwa ajili ya kupisha mazungumzo kati ya klabu za Simba na Eskilstuna  ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka.
uongozi wa Simba umekiri kufurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, huku ukisisitiza kutokusita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi. klabu na Taifa kwa ujumla.
Katika hatu nyingine  kesho uongozi wa klabu ya Simba utakutana na viongozi wote wa matawi ya Dar es salaam.
Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.
Wakati huo huo uongozi wa klabu ya SImba umewaomba wanachama na mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa.

Video: JPM apigilia msumari mwingine jengo la Tanesco Ubungo
Uamuzi wa kamati kuhusu usajili ligi ya wanawake